Dada zangu naomba niandike kwa sauti kubwa kabisa mnielewe maana aisee mnadanganyika na uongo mwingine mpaka mnanpia hasira ipo siku nitavunja simu yangu hapa na hali ilivyo ngumu! Iko hivi, kama una mpenzi wako, mpo kwenye mahusiano kwa zaidi ya miezi mitatu, narudia zaidi ya miezi mitatu, hajawahi kukupeleka kwake, mechi anataka mkapigie gest au nyumbani kwako.
Ukitaka kwenda kwake anaanza sijui pale wambea wengi, mara bado naishi kwetu, mara naishi na wadogo zangu, mara kuna wageni wengi sijui nini? Kuna mwingine kaambiwa eti nyumba ina choo cha nnje utasumbuka na yeye akaamini. Unakuta mwanaume anakupa visababau sababu vya kijinga jinga ambavyo havieleweki, mwanaume anafanya kazi lakini hataki kabisa ujue kwao.
Hata ukimuambia kuwa nionyeshe basi nyumba ilipo hata kama sitafika niingie hataki. Lakini sasa na hapa ndiyo mnadanganywa mwanaume huyu huyu unaweza kumpigia simu hata saa nane usiku tena wakati mwingine Video call basi huyu ana mke kabisa au mwanamke anaishi naye. Wanaume wengi waliooa ndiyo wanaongoza kuongea usiku, tena sio kwamba wake zao wamesafiri, hapana wapo na hawajali, mwanamke kashaongea mpaka kachoka, nimeandika ili siku likikukuta usijesema sijakuambia, kuwa makini na mwanaume huyu!

Comments
Post a Comment