Skip to main content

ASILIMIA 90 YA MANENO WAKATI UNATONGOZWA NI UONGO

Wakati wakutongozwa mkubali mwanaume kwakua amekuvutia, ukimuangalia unasema huyu tunaweza kuvumiliana hata katika mahusiano, kwakua anakuheshimu kwamba anapoongea na wewe haongei kauli za dharau na kishenzi na tatu kwakua yuko salama kiafya (sasa hapa ni kama na wewe upo tayari kupima) ila ukimkubali mwanaume kwakua alikuambia sijui  nini, sijui yuko siriasi anataka kuoa, sijui katoka kuumizwa, sijui anakupenda basi jua imekula kwako.

Asilimia 90 ya maneno wanaume wengi wanayoongea wakati wanatongoza ni uongo. Kuna utongozaji wa namna mbili, aina ya kwanza ni kutongoza mwanamke usiyemjua, huyu umekutana naye kwenye Basi, mtaani, anapita njia na popote humjui hakujui, hapa unatumia ubaharia, unaonyesha tabia njema ukikisia labda anapenda hii na kile, unamsoma vizuri mwanamke na unamuacha ajiongeze mwenyewe.

Mmabaharia tunajua kuwa ukimuacha mwanamke kuongea atakuambia kila kitu anachokipenda mara “Ohhh mimi nishaumizwa sana… nataka mtu siriasi ..nilikua na mahusiano na mwanaume blah blah blah…. Mara hivi napenda kile” Unamuacha anaongeawee kisha ukifungua mdomo ushajua anataka nini unaanza kuigiza kile anachotaka. Kama kakuambia kaumizwa unampa namna ulivyoachana na X wako baada ya kumfumania, namna ulivyokua unamhudumia X wako lakini hana shukurani…namna ulivyoachana na mke wako kwakua alikuahampendi Mama yako na utumbo utumbo mwingi dada anaona mwanaume ndiyo huyu!

Aina ya pili ya kutongoza ni kwa mwanamke unayemjua, huyu unafungua mafaili yake, labda n rafiki yako unajua kuwa katoka kuumizwa, labda anapenda pesa, mtu wa kulialia anataka ndoa na vingine. Labda unamjua rafiki yake, unamuuliza anakupa mafaili yote, ukienda kumtongoza tayari ushajua na uongo wa kumpa lazima ataingia laini tu kwakua unaenda na majibu. Kama ulikua hujui hii mbinu hata kama wewe si baharia ni rahisi na dada zangu unaweza kukutana na mwanaume unaona kila kitu uanchotaka ndiyo yeye.

Yaani mpaka unahisi Mungu kamshusha kwani hujamuambia kuhusu ndoa kashaanza kuongea mambo ya kuoakuoa usiriasi, mambo ya kutaka kutulia sijui na mipango kibao mpaka unasahau kadanga kako. Dada kama unasoma hapa na ukamkubali mwanaume sababu ya ahadi zake basi kapimwe ubongo wako. Watu wanakesha kufuatilia mafaili yako, akija kwakoa nakupa majibu, na wengine mnasema wenyewe napenda hiki napenda mwanaume anayepiga simu, anayefanya hivi, anayefanya vile sasa kwanini asifanye, ila akishakupata sasa kwaninia igize tena, Kuku ushamchinja kwanini uhangaike tena kumrushia Mahindi?

Mimi nishamaliza, wewe katongozwe, sijakuambia umedanganywa kuhusu ndoa ila nakuambia wanaume ni waongo hivyo kuwa makini endelea kufuatilia na mtag basi na rafiki yako

Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO YA UZAZI | TASA

MIZIZI YA MKUNDE PORI NA FAIDA ZAKE ■ Inasafisha kizazi ■ Inazibua mirija iliyoziba ■ Inaondoa sumu kwa wale waliotumia sindano za uzazi/vidonge vya uzazi. ■ Inakomaza mayai kwa wale wenye tatizo la mayai kutokukomaa na kusababisha mayai kutokupevuka ■ Inasogeza kizazi karibu kwa wale ambao vizazi vyao vipo mbali ■ Majani ya mkunde pori pia ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume • Dalili mojawapo itakayokufanya ujue dawa hii ya mkunde pori inafanya kazi ni kwenda haja ndogo mara nyingi kuliko kawaida. • Dalili nyingine ni tumbo kuvuta sana chini ya kitovu. Usipoona dalili hizi usiogope maana ukubwa wa tatizo unatofautiana. ANGALIZO KWA WANAWAKE WATAKAOTUMIA KWA AJILI YA UZAZI, Ukinywa dawa hii hakikisha siku za hatari unakutana na mwenzi wako...na baada ya hapo usitumie dawa mpaka upime mimba kwanza maana mimba nyingine dalili zake huchelewa kuonekana hivyo unaweza ukanywa tena mimba kama imeingia ikatoka. Wajawazito hawaruhusiwi kutumia. MATUMIZ CHUKUA MIZIZ...

RAHA YA KUWA NA MWANAMKE MWEUSI KWENYE MAHUSIANO

Nilikuwaga sielewi kwanini hawa wanawake weusi aka blacks wanasifiwa sana?. Jaman hii type ni raha sana kudate nayo unakuwa huna stress kwanza hawana vizinga vya kizembe zembe, wanaridhika hata wakipewa kitu kidogo, yani wanajua kupenda na wengi wana true love. Sijamaliza bado, wanawake weusi wanajua nini maana ya mapenzi, wanajua kukaa na mwanaume halafu pia wanajituma sana akija ghetto anafanya kila kitu hadi kubrash viatu.  Ukija kwenye kule kwa 6x6 sio wachoyo kukupa na wanajua balaa ni mafundi na hawana maringo kabisa.  Shida ya hizi rangi nyeupe ni kwamba zina maringo sana na wanavizinga sana unakuta dada kaupele kadogo kameota anataka dawa halafu utasikia 50k dawa ya uson wtf?? Hawa mademu weupe wana vizinga sana halafu wengi ni malaya sana. Nasema haya coz me nilikuwa mhanga sana wa hizi type nyeupe ila toka nianze kula hizi nyeusi mmeona utofauti mkubwa sana mpaka nimeanza kuwaelewa mablacks yani hawana complications. Popote mlipo nyie wanawake weusi agizen...

USIMUAMINI KAMWE....!!

Dada zangu naomba niandike kwa sauti kubwa kabisa mnielewe maana aisee mnadanganyika na uongo mwingine mpaka mnanpia hasira ipo siku nitavunja simu yangu hapa na hali ilivyo ngumu! Iko hivi, kama una mpenzi wako, mpo kwenye mahusiano kwa zaidi ya miezi mitatu, narudia zaidi ya miezi mitatu, hajawahi kukupeleka kwake, mechi anataka mkapigie gest au nyumbani kwako. Ukitaka kwenda kwake anaanza sijui pale wambea wengi, mara bado naishi kwetu, mara naishi na wadogo zangu, mara kuna wageni wengi sijui nini? Kuna mwingine kaambiwa eti nyumba ina choo cha nnje utasumbuka na yeye akaamini. Unakuta mwanaume anakupa visababau sababu vya kijinga jinga ambavyo havieleweki, mwanaume anafanya kazi lakini hataki kabisa ujue kwao. Hata ukimuambia kuwa nionyeshe basi nyumba ilipo hata kama sitafika niingie hataki. Lakini sasa na hapa ndiyo mnadanganywa mwanaume huyu huyu unaweza kumpigia simu hata saa nane usiku tena wakati mwingine Video call basi huyu ana mke kabisa au mwanamke anaishi naye. Wan...