Skip to main content

JE NI POA KUPASHA KIPORO NA MPENZI WAKO WA ZAMANI

Hakuna dharau kubwa kwa mwanamke kama vile mwanaume ambaye alikua mpenzi wako halafu akaoa mwanamke mwingine halafu anarudi kwako anakuambia bado anakupenda anataka kufanya tena mapenzi na wewe. Hapa naamanisha bila kujali sababu za yeye kukuacha kama alikuacha na kwenda kuoa mwingine halafu bado anakutumia kingono basi jua kuwa sio kwamba anakupenda na anashindwa kukusahau hapana ni kwamba amekudharau na anakuona mpumbavu.

Hata kama alikuacha kwakua mmetofautiana Dini, hata kama alikatazwa na wazazi wake hata kama ni wewe ulimuacha, lakini kama mliachana na akarudi kutembea na wewe baada ya kuoa basi jua kuwa kakudharau. Kwanza kabisa anajua kabisa hujithamini ndiyo maana kwako anakua kimwili na kwa mkewe anaenda kutengeneza maisha. Lakini ni kama anajihakikishia kuwa huyu si mwanamke wa kuoa kabisa na alifanya maamuzi sahihi.

Iko hivi moja ya wanawake ambao wanaume huwadharau ni wanawake ambao wanatembea na waume za watu tena bila malengo. Lakini atakua amekuona mpuuzi kabisa kama wewe utakua umeolewa na mwanaume mwingine halafu ukarudiana na yeye, huyu mwanaume hatakuheshimu na kwani anajau kua huithamini ndoa yako.

Hata kama ikitokea ukaachika kwa mume wako basi jua kuwa kama livyokuacha mara ya kwanza na kuoa mwingine hatamuacha mkewe kwaajili yako. Hii ni kwasababu anajua kuwa wewe si mtu wa kuaminika ni kicheche. Wanaume tunapenda sana kusaliti lakini si kusalitiwa. Anajua kuwa kama ulimsaliti mumeo na X wako basi hata yeye unaweza kumsaliti na X wako hivyo ni vigumu sana kuendelea na mahusiano baada ya kuona umeachika.

Najua unadhani unamkomoa mke wake, tena kwakua anaonyesha kukujali kuliko mkewe, hata wakati mwingine kutumia muda mwingi na wewe na kumtukana au kumnyanyasa mbele yako ukafikiri wewe una thamani zaidi. Hapana anajifanya nikua anakuridhisha tu, anajua mkewe hawezi kuondoka hivyo ili kukushikilia wewe na kuendelea kukutumia nilazima aonyeshe kama vile anakujali wewe zaidi kuliko mkewe ili usiondoke!

Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO YA UZAZI | TASA

MIZIZI YA MKUNDE PORI NA FAIDA ZAKE ■ Inasafisha kizazi ■ Inazibua mirija iliyoziba ■ Inaondoa sumu kwa wale waliotumia sindano za uzazi/vidonge vya uzazi. ■ Inakomaza mayai kwa wale wenye tatizo la mayai kutokukomaa na kusababisha mayai kutokupevuka ■ Inasogeza kizazi karibu kwa wale ambao vizazi vyao vipo mbali ■ Majani ya mkunde pori pia ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume • Dalili mojawapo itakayokufanya ujue dawa hii ya mkunde pori inafanya kazi ni kwenda haja ndogo mara nyingi kuliko kawaida. • Dalili nyingine ni tumbo kuvuta sana chini ya kitovu. Usipoona dalili hizi usiogope maana ukubwa wa tatizo unatofautiana. ANGALIZO KWA WANAWAKE WATAKAOTUMIA KWA AJILI YA UZAZI, Ukinywa dawa hii hakikisha siku za hatari unakutana na mwenzi wako...na baada ya hapo usitumie dawa mpaka upime mimba kwanza maana mimba nyingine dalili zake huchelewa kuonekana hivyo unaweza ukanywa tena mimba kama imeingia ikatoka. Wajawazito hawaruhusiwi kutumia. MATUMIZ CHUKUA MIZIZ...

RAHA YA KUWA NA MWANAMKE MWEUSI KWENYE MAHUSIANO

Nilikuwaga sielewi kwanini hawa wanawake weusi aka blacks wanasifiwa sana?. Jaman hii type ni raha sana kudate nayo unakuwa huna stress kwanza hawana vizinga vya kizembe zembe, wanaridhika hata wakipewa kitu kidogo, yani wanajua kupenda na wengi wana true love. Sijamaliza bado, wanawake weusi wanajua nini maana ya mapenzi, wanajua kukaa na mwanaume halafu pia wanajituma sana akija ghetto anafanya kila kitu hadi kubrash viatu.  Ukija kwenye kule kwa 6x6 sio wachoyo kukupa na wanajua balaa ni mafundi na hawana maringo kabisa.  Shida ya hizi rangi nyeupe ni kwamba zina maringo sana na wanavizinga sana unakuta dada kaupele kadogo kameota anataka dawa halafu utasikia 50k dawa ya uson wtf?? Hawa mademu weupe wana vizinga sana halafu wengi ni malaya sana. Nasema haya coz me nilikuwa mhanga sana wa hizi type nyeupe ila toka nianze kula hizi nyeusi mmeona utofauti mkubwa sana mpaka nimeanza kuwaelewa mablacks yani hawana complications. Popote mlipo nyie wanawake weusi agizen...

USIMUAMINI KAMWE....!!

Dada zangu naomba niandike kwa sauti kubwa kabisa mnielewe maana aisee mnadanganyika na uongo mwingine mpaka mnanpia hasira ipo siku nitavunja simu yangu hapa na hali ilivyo ngumu! Iko hivi, kama una mpenzi wako, mpo kwenye mahusiano kwa zaidi ya miezi mitatu, narudia zaidi ya miezi mitatu, hajawahi kukupeleka kwake, mechi anataka mkapigie gest au nyumbani kwako. Ukitaka kwenda kwake anaanza sijui pale wambea wengi, mara bado naishi kwetu, mara naishi na wadogo zangu, mara kuna wageni wengi sijui nini? Kuna mwingine kaambiwa eti nyumba ina choo cha nnje utasumbuka na yeye akaamini. Unakuta mwanaume anakupa visababau sababu vya kijinga jinga ambavyo havieleweki, mwanaume anafanya kazi lakini hataki kabisa ujue kwao. Hata ukimuambia kuwa nionyeshe basi nyumba ilipo hata kama sitafika niingie hataki. Lakini sasa na hapa ndiyo mnadanganywa mwanaume huyu huyu unaweza kumpigia simu hata saa nane usiku tena wakati mwingine Video call basi huyu ana mke kabisa au mwanamke anaishi naye. Wan...