Skip to main content

KAMA UNASUBIRI AMUACHE TARATIBU UTASHUHUDIA AKIMUOA TARATIBU!

Ubaya wa wanawake ni wagumu kuelewa, wakishapenda wanadhani kuwa mapenzi yanatosha, ipo hivi mapenzi yanatosha kama wote mnapendana. Ukikutana na mwanaume akakuambia kuwa “Nina mtu lakini nataka kumuacha polepole ili nisimuumize!” Basi jua kuwa huyo mtu hakupendi na anachotaka ni kuchepuka kwa uhuru, kwanza wewe ndiyo mchepuko ndiyo maana huyo mwingine hataki kumuumiza, hakuna cha kuacha taratibu na hakuna namna ambayo unaweza kumuacha mtu bila kumuumiza kama kweli alikua anakupenda!

Kwanza kuacha polepole ndiyo nini kwamba unamkaanga au unamuacha kwa kumuwekea kachumbari! Ni sawa na kusema eti namchinza polepole tena ndiyo yenye maumivu makali zaidi, hembu fikiia unamchinja kuku polepole, unajua kuwa atakufa lakini unamchinja polepole. Kwanza niseme kuwa wewe unayeambiwa na ukakubali kuwa mwenzako aache polepole na huyo anayekuambia kuwa anaacha polepole wote ni washenzi tu, narudia wote ni washenzi tu! Hembu fikiria upo na mwanaume.

Unajua anakupenda kumbe anakuacha polepole, kwamba kila sikua anakuja kwako, kila siku anakutumia meseji, anakuambia hana mtu anakudanganya atakuoa unabeba na mimba yake kumbe mwenzako ana mtu wake na washakubaliana kuwa wakuache polepole. Anakupotezea muda, unakaa miaka miwili na mwanaume anayekuacha polepole, unakataa wachumba, unakataa madanga kisa una mtu wako anayekuambia kuwa anakuacha polepole, si ushenzi huo. Nashindwa hata kuwalewa nyie wanawake mnaoambiwa hivyo.

Uko na mwanaume anakuambia nina mtu naishi naye nitamuacha polepole, nina mke, mpenzi, nimezaa naye, kwamba hiyo polepole wanakua wanafanya mapenzi nusunusu au? Mwanaume akikuambia hivyo basi jua kuwa huyo mwanaume ni MSHENZI na kakudharau, lakini wewe ukikubali hivyo basi jitafutie tusi mwenyewe kwani unadanganywa! Hakuna kitu kama hicho, ukiona unaambiwa hivyo jua huyo mwanaume hakupendi wewe ni mchepuko narudia wewe ni mchepuko na kama ni mume wako basi jua kashafikia kiwangi kikubwa cha umalaya wala hajali kama wewe ni mkewe au binamu yake!

Najua kuna wengi imewachoma ila hamna namna ndiyo ukweli, sasa wewe jibeshe mimba ukisubiria amuache taratibu ukishtuka utakuta kamuoa taratibu!

Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO YA UZAZI | TASA

MIZIZI YA MKUNDE PORI NA FAIDA ZAKE ■ Inasafisha kizazi ■ Inazibua mirija iliyoziba ■ Inaondoa sumu kwa wale waliotumia sindano za uzazi/vidonge vya uzazi. ■ Inakomaza mayai kwa wale wenye tatizo la mayai kutokukomaa na kusababisha mayai kutokupevuka ■ Inasogeza kizazi karibu kwa wale ambao vizazi vyao vipo mbali ■ Majani ya mkunde pori pia ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume • Dalili mojawapo itakayokufanya ujue dawa hii ya mkunde pori inafanya kazi ni kwenda haja ndogo mara nyingi kuliko kawaida. • Dalili nyingine ni tumbo kuvuta sana chini ya kitovu. Usipoona dalili hizi usiogope maana ukubwa wa tatizo unatofautiana. ANGALIZO KWA WANAWAKE WATAKAOTUMIA KWA AJILI YA UZAZI, Ukinywa dawa hii hakikisha siku za hatari unakutana na mwenzi wako...na baada ya hapo usitumie dawa mpaka upime mimba kwanza maana mimba nyingine dalili zake huchelewa kuonekana hivyo unaweza ukanywa tena mimba kama imeingia ikatoka. Wajawazito hawaruhusiwi kutumia. MATUMIZ CHUKUA MIZIZ...

RAHA YA KUWA NA MWANAMKE MWEUSI KWENYE MAHUSIANO

Nilikuwaga sielewi kwanini hawa wanawake weusi aka blacks wanasifiwa sana?. Jaman hii type ni raha sana kudate nayo unakuwa huna stress kwanza hawana vizinga vya kizembe zembe, wanaridhika hata wakipewa kitu kidogo, yani wanajua kupenda na wengi wana true love. Sijamaliza bado, wanawake weusi wanajua nini maana ya mapenzi, wanajua kukaa na mwanaume halafu pia wanajituma sana akija ghetto anafanya kila kitu hadi kubrash viatu.  Ukija kwenye kule kwa 6x6 sio wachoyo kukupa na wanajua balaa ni mafundi na hawana maringo kabisa.  Shida ya hizi rangi nyeupe ni kwamba zina maringo sana na wanavizinga sana unakuta dada kaupele kadogo kameota anataka dawa halafu utasikia 50k dawa ya uson wtf?? Hawa mademu weupe wana vizinga sana halafu wengi ni malaya sana. Nasema haya coz me nilikuwa mhanga sana wa hizi type nyeupe ila toka nianze kula hizi nyeusi mmeona utofauti mkubwa sana mpaka nimeanza kuwaelewa mablacks yani hawana complications. Popote mlipo nyie wanawake weusi agizen...

USIMUAMINI KAMWE....!!

Dada zangu naomba niandike kwa sauti kubwa kabisa mnielewe maana aisee mnadanganyika na uongo mwingine mpaka mnanpia hasira ipo siku nitavunja simu yangu hapa na hali ilivyo ngumu! Iko hivi, kama una mpenzi wako, mpo kwenye mahusiano kwa zaidi ya miezi mitatu, narudia zaidi ya miezi mitatu, hajawahi kukupeleka kwake, mechi anataka mkapigie gest au nyumbani kwako. Ukitaka kwenda kwake anaanza sijui pale wambea wengi, mara bado naishi kwetu, mara naishi na wadogo zangu, mara kuna wageni wengi sijui nini? Kuna mwingine kaambiwa eti nyumba ina choo cha nnje utasumbuka na yeye akaamini. Unakuta mwanaume anakupa visababau sababu vya kijinga jinga ambavyo havieleweki, mwanaume anafanya kazi lakini hataki kabisa ujue kwao. Hata ukimuambia kuwa nionyeshe basi nyumba ilipo hata kama sitafika niingie hataki. Lakini sasa na hapa ndiyo mnadanganywa mwanaume huyu huyu unaweza kumpigia simu hata saa nane usiku tena wakati mwingine Video call basi huyu ana mke kabisa au mwanamke anaishi naye. Wan...