Skip to main content

KAMA UPO NAE ZAIDI YA MIAKA 3 MUULIZE SIO KWA KULALAMIKA

Kama upo kwenye mahusiano na mwanaume miaka mitatu na haeleweki basi ukimaliza kusoma hapa muulize sio kwa kulalamika, kwa kumuangalia usoni muulize hivi una mpango wa kunioa au unanipotezea muda wangu tu. Acha kudhani kwakua anakuambia anakupenda atakuoa, acha kudhani kwakua amekuambia mfungue biashjara ya pamoja atakuoa, acha kudhani kwakua amekuambia umzalie atakuoa, acha kudhani kwakua mnaishi pamoja atakuoa, acha kudhani kwakua ulimtafutia kazi atakuooa.

Acha kudhani kwakua ndugu zake wanakujua anakuacha uongee na Mama yake atakuoa. Acha kudhani kwakua anakusifia kua wewe ni wife material atakuoa. Muulize tena acheni lile swali la “Kwetu utakuja lini kujitambulisha?” Ndugu yangu aje kwanu kakuambia anakutaka, au alishaweka ahadi muulize uso mkavu kama umepiga cha arusha “Hivi una mpango wa kunioa au huna?” inawezekana hajafikia kuoa lakini ana mpango na wewe au amefikia lakini hana mpango na wewe.

Miaka mitatu ni mingi kwa mtu kukuchunguza tabia, labda kama anataka kujua na maini yako yaje au kuchunguza namna utumbo wako ulivyojinyongorokota! Ila nataka mnielewe, miaka mitatu haihusu mapenzi ya utoto kipindi mko sekondari au chuo,. Miaka mitatu haihuishi kipindi ambacho mwanaume kamaliza chuo hana kazi. Hapana, miaka mitatu haihusu wale ambao mnatembea na vivulana, vina miaka 30 lakini vipo kwao na havina mpango hata wakuondoka.

Ukitaka kuhesabu miaka mitatu angalia miaka ambayo kamaliza chuo, kapata kazi, kaakaa miaka miwili kazini kisha hesabu mitatu baada ya yeye kupata kazi na kuwa mwanaume. Sio mtu hana kazi hata kama mko naye miaka kumi unataka akuoe, akupeleke wapi? Kwanza mwanaume akiwa bado hajapata pesa huwezi jua hata anakupenda, inawezekana hata yuko na wewe kwakua ana shida tu akipata pesa anamfuata yule dada mwingine sijui nani halafu unaulizia akuoe lini?

Hii pia haiwahusu wale wadada ambao mnafanya kazi lakini badala ya kusaidia ndugu zenu mmechukua mwanaume mtu mzima mmemuweka ndani mnamhudumia, nyie subirini kuiachika akishapata pesa! Unataka akuoe nini wakati ushamuoa? Unamhudumia mwanaume kila kitu halafu unataka akuoe? Yaani mtu ambaye hata yeye mwenyewe hawezi kujihudumia unataka aoe ili? Unajua anaandika sana , sijui kama mmenielewa, ila kama haeleweki miaka mitatu basi hataeleweka kumi, sisemi hatakuoa lakini ishi kwa tahadhari usijiozeshe kisa mmeishi sita ukaanza kumuita mume!

Najua inaume kwakua ulishawekeza nguvu nyingi sana kwake ila sasa mimi nifanyeje, hamna namna fuatilia blog yangu kila siku kufahamu mengi zaidi

Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO YA UZAZI | TASA

MIZIZI YA MKUNDE PORI NA FAIDA ZAKE ■ Inasafisha kizazi ■ Inazibua mirija iliyoziba ■ Inaondoa sumu kwa wale waliotumia sindano za uzazi/vidonge vya uzazi. ■ Inakomaza mayai kwa wale wenye tatizo la mayai kutokukomaa na kusababisha mayai kutokupevuka ■ Inasogeza kizazi karibu kwa wale ambao vizazi vyao vipo mbali ■ Majani ya mkunde pori pia ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume • Dalili mojawapo itakayokufanya ujue dawa hii ya mkunde pori inafanya kazi ni kwenda haja ndogo mara nyingi kuliko kawaida. • Dalili nyingine ni tumbo kuvuta sana chini ya kitovu. Usipoona dalili hizi usiogope maana ukubwa wa tatizo unatofautiana. ANGALIZO KWA WANAWAKE WATAKAOTUMIA KWA AJILI YA UZAZI, Ukinywa dawa hii hakikisha siku za hatari unakutana na mwenzi wako...na baada ya hapo usitumie dawa mpaka upime mimba kwanza maana mimba nyingine dalili zake huchelewa kuonekana hivyo unaweza ukanywa tena mimba kama imeingia ikatoka. Wajawazito hawaruhusiwi kutumia. MATUMIZ CHUKUA MIZIZ

RAHA YA KUWA NA MWANAMKE MWEUSI KWENYE MAHUSIANO

Nilikuwaga sielewi kwanini hawa wanawake weusi aka blacks wanasifiwa sana?. Jaman hii type ni raha sana kudate nayo unakuwa huna stress kwanza hawana vizinga vya kizembe zembe, wanaridhika hata wakipewa kitu kidogo, yani wanajua kupenda na wengi wana true love. Sijamaliza bado, wanawake weusi wanajua nini maana ya mapenzi, wanajua kukaa na mwanaume halafu pia wanajituma sana akija ghetto anafanya kila kitu hadi kubrash viatu.  Ukija kwenye kule kwa 6x6 sio wachoyo kukupa na wanajua balaa ni mafundi na hawana maringo kabisa.  Shida ya hizi rangi nyeupe ni kwamba zina maringo sana na wanavizinga sana unakuta dada kaupele kadogo kameota anataka dawa halafu utasikia 50k dawa ya uson wtf?? Hawa mademu weupe wana vizinga sana halafu wengi ni malaya sana. Nasema haya coz me nilikuwa mhanga sana wa hizi type nyeupe ila toka nianze kula hizi nyeusi mmeona utofauti mkubwa sana mpaka nimeanza kuwaelewa mablacks yani hawana complications. Popote mlipo nyie wanawake weusi agizeni mirinda

STORI YANGU; NILIZAA NA WEWE KWAKUA UNAWEZA KUHUDUMIA MTOTO!

Wote tuliingia kazini siku moja, mimi niliajiriwa kama afisa mikopo wakati yeye aliajiriwa kama mhasibu lakini wote tulianzia kama mateila mpaka baada ya kama miezi sita hivi ndiyo tulitoka na kila mtu akawa ameenda katika kitengo chake.  Kuna dada mwingine ambaye walikua kitengo komoja na wote tulikua marafiki. Mimi ni msiri sana hivyo hata nilipoanzisha mahusiano yangu na Kelvin (Sio jina lake halisi) sikumuambia mtu yoyote zaidi ya Edna ambaye ingawa tulikutana kazini lakini alishaanza kuwa kama Dada yangu. Edna alikua ni rafiki yangu mkubwa, anakuja nyumbani kwangu tunaongea na nilimsaidia katika mambo mengi. Wakati Mama yake anaumwa kalazwa hospitali nakumbuka aliishiwa kabisa, hata kodi ya nyumba alikosa, walitaka kumfukuza lakini nikatoa pesa yangu laki tisa na kumlipia, baadaye alipotaka kunirudishia nilimuambia hapana. Alishukuru sana, kwa upande wa Kelvin mahusiano yetu yalikua hatakaharaka, tulifanya karibu kila kitu pamoja. Wakati nanunua kiwanja ili kujenga yeye ali