Skip to main content

STORI YANGU; NILIZAA NA WEWE KWAKUA UNAWEZA KUHUDUMIA MTOTO!


Wote tuliingia kazini siku moja, mimi niliajiriwa kama afisa mikopo wakati yeye aliajiriwa kama mhasibu lakini wote tulianzia kama mateila mpaka baada ya kama miezi sita hivi ndiyo tulitoka na kila mtu akawa ameenda katika kitengo chake.  Kuna dada mwingine ambaye walikua kitengo komoja na wote tulikua marafiki. Mimi ni msiri sana hivyo hata nilipoanzisha mahusiano yangu na Kelvin (Sio jina lake halisi) sikumuambia mtu yoyote zaidi ya Edna ambaye ingawa tulikutana kazini lakini alishaanza kuwa kama Dada yangu.

Edna alikua ni rafiki yangu mkubwa, anakuja nyumbani kwangu tunaongea na nilimsaidia katika mambo mengi. Wakati Mama yake anaumwa kalazwa hospitali nakumbuka aliishiwa kabisa, hata kodi ya nyumba alikosa, walitaka kumfukuza lakini nikatoa pesa yangu laki tisa na kumlipia, baadaye alipotaka kunirudishia nilimuambia hapana. Alishukuru sana, kwa upande wa Kelvin mahusiano yetu yalikua hatakaharaka, tulifanya karibu kila kitu pamoja.

Wakati nanunua kiwanja ili kujenga yeye alikua hana mpango kabisa wa kujenga, nilimshawishi naye akanunua kiwanja karibu yangu. wakati naanza ujenzi alitaka tujenge pamoja lakini nilimuambia kuwa itakua ni busara kila mtu kujengha kivyake. Tulianza ujenzi lakini yeye alikua anasuasua, mimi tayari nilishaanza kuuza vitenge, nilikua nikiagiza jumla nauza kwenye mitandao na kutuma kwa marafiki zangu, nilikua nikipata pesa nyingi tu.

Lakini kuna shamba la mpunga ambalo nilinunua Ifkara kipindi nasoma A-Level, nilibana pesa ya matumizi na kununua kipindi hicho hivyo nilitafuta mtu akawa anasimamia na kuanza kulima. Nilivuna vizuri, huyo mtu akawa ananikusanyia na mpuga hivyo nilipata faida kubwa tu, kwakua nilijua kipato chake si kikubwa sana nilikua nikimsaidia sana, nilikua nikinunua vifaa na mnunulia na vyake, vikibaki napa nayeye, lengo lilikua ni kumaliza kujega pamoja ilia sijisikie vibaya. Alipoona mimi nafanikiwa alitaka tufanye Biashara pamoja kwamba tununue vitenge pamoja na kuuza pamoja.

Nilijua kabisa kuwa ni uoga wa Biashara aliokuanao hjivyo nilimsahawishi trufungue Biashara nyingine mini-supermarket ambayo ina jina lake. Mimi nilimchangia mtaji kama milioni tatu hivi na yeye akatoa tano. Ilianza vizuri na kila kitu nilikua nasimamia mimi kwani alikua hawezi, baishara ilipanuka haraka haraka kwani kwa pale ilikua ni kama kitu kipya kabisa. Mambo yaliendelea vizuri, kwaja juzi mwishoni aliniambia kuwa anataka tuzae, mimi nilimuliza ni kwanini? Kama ni ishu ya mtoto ni kwanini tusifunge ndoa kwanza.

Alikaa kimya na kuipotezea akiniambia kuwa hajajipanga, lakini baada ya kama miezi mitatu baaddaye aliniambia kuwa anataka kuoa. Nilimuambia ni jambo zuri, hakuniambia anataka kumuoa nani lakini niliona kama vile amebadilika flani, ukaribu wa zamani haupo, nilimuuliza nini tatizo akaniambia kuwa anataka mtoto na mimi ila anaona kama vile mimi siko tayari. Aliniambia kuwa anataka nibebe mimba kwanza ili akienda kujitambulisha tunafunga ndoa harahaharaka na tunaanza familia,a likua hataki tuoane tuko kwenye ndoa ndiyo kuanza mchakato wa kutafuta mtoto.

Kwakua nilikua nampenda nilibeba mimba yake na namshukuru Mungu kwaka jana mwezi wa nane nilijifungua mtoto wakike. Wakati wa ujauzito kila kitu kilikua sawa lakini nilipomuambia suala la kujitambulisha alikua akipiga chenga na kutoa sababu ambazo hazieleweki. Kwakua sikutaka kuonekana kuwa nina shida sana ya ndoa nilivumilia, mwaka huu mwezi wa pili mimi nilipanishwa cheo na mshahara kidogo, wote tulifurahia. Lakini mwezi wa pili mwaka huu nilikua nimesafiri kikazi, ilikua ni safari ya wiki mbili.

Nikiwa huko nilipigiwa sim kuwa Kelvin anaoa, nilishangaa sana, mtu aliyenipigia alikua ni Mama mtu mzima lakini sikumuamini. Nilimkubalia tu sawa,  aliniuliza unajua anamuoa nani sikujibu kwani sikua nikijua hata  alikua anaoa, ndipo aliniambia kuwa anamuoa Edna ambaye alikua ni rafiki yangu kupika na kupakua, kila kitu changu namuambia yeye tunashauriana, Biashara aliyofungua ni mimi nilimsaidia na mambo mengi ya kazini mimi ndiyo namsaidia. Nilishtuka, niliumia lakini bado sikuamini, niliona kama vile watu wananichezea.

“Hawawezi kunifanyia hivi, hati hata kama angekua anaoa mtui mwingine.” Niliwaza, nilirudi kwenye semina bila kumuuliza chochote, niliendelea na maisha yangu lakini sasa nikichunguza nyendo zao, sikutaka kukurupuka na kuulizia kwani niliona kama ni uongo basi nitakua nimemkosea mpenzi wangu. Mwezi wa nne mwaka huu kuna mtu alinifuata kabisa kuwa Kelvin kaenda kutoa mahari kwa kina Edna na ndoa ni mwaka huu mezi wa tisa. Hapo nilishtuka kidogo kwani kipindi hicho Edn alikua likizo alikua kwao na Kelvin alisafiri kwa ruhusa.

Nilichanganyikiwa lakini nilijikaza, aliporudi alishukia kwangu kama kawaida, ilikua kama hakuna kitu kimetokea. Nilishindwa kuvumilia na kumuuliza, lakini cha ajabu alikaaka katakata kuwa hakuna kitu kama hicho. Alikua mkali, akaniambia mimi nasikiliza sana watu, akaongea maneno mengi akisema kama nimemchoka basi nimuache na si kumsingizia vitu kama hivyo. Mimi nilinyamaza na kuomba msamaha lakini riho haikua na aman, nilimuuliza Edna kwa kumpigia simu lakini naye alikana katakata.

Baada ya kuona hivyo nilikaa kimya, lakini wiki moja iliyopita Kelvin alinitumia meseji “Mimi naona bora tuachane, mapenzi yetu hayaelekei popote tulee tu mtoto.” Nilipaniki sana nikamfuata kwake na kumuuliza kwanini anataka kuniacha, ndipo aliniambia kuwa ni kweli anamuoa Edna mwezi wa tisa na walikua kweye mahusiano kwa muda na anaona yeye ndiyo mwanamke sahihi kwake. Nilimuuliza kosa langu ni nini akakaa kimya, aliishia tu kuniomba msamaha lakini sikukubali, nilitaka kujua kosa langu mimi ni nini?

“Tatizo lako ni kama mwanaume, una akili sana, kila kitu unachokifanya unafanikiwa mpaka mimi najiona kama ni mwanamke. Angalia vitu vyote hivi nilivyonavyo ni wewe umenishauri, hapana siwezi kukuoa.” Aliniambia maneno ambayo yaliniumiza sana na mpaka leo yananiumiza sijui chakufanya, yaani ananiacha kwakua tu nina akili kumzidi. Nilimuliza sasa kama alijua hivyo ni kwanini alinidanganya tuzae pamoja. “Najua wewe ni mtafutaji, nilijua nikizaa na wewe mtoto wetu hatapata shida unaweza kumlea mwenyewe.”

Aliniambia huku akijaribu kunikumbatia kunipa moyo, nilijitoa mikononi mwake. “Pole kwakukuumiza lakini mimi na Edna sasa ni wachumba nisamehe…” Aliongea, nilijikuta naishiwa nguvu na kudondoka, sikupoteza fhamu, alitaka kuninyanyua lakini nilimkatalia, nilijikongoja nikanyanyuka, nikachukua Bajaji mpaka kwangu. kesho nilishindwa hata kwenda kazini mpaka leo sijaenda wanajua naumwa lakini cha ajabu mpaka sasa hajanitafuta bado nimechanganyikiwa naumia sijui hata chakufanya kwani nikirudi kazini naenda kukutana nao wote.

MWISHO; Kwa simulizi kama hizi hakikisha unafuatilia Iddi Makengo

Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO YA UZAZI | TASA

MIZIZI YA MKUNDE PORI NA FAIDA ZAKE ■ Inasafisha kizazi ■ Inazibua mirija iliyoziba ■ Inaondoa sumu kwa wale waliotumia sindano za uzazi/vidonge vya uzazi. ■ Inakomaza mayai kwa wale wenye tatizo la mayai kutokukomaa na kusababisha mayai kutokupevuka ■ Inasogeza kizazi karibu kwa wale ambao vizazi vyao vipo mbali ■ Majani ya mkunde pori pia ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume • Dalili mojawapo itakayokufanya ujue dawa hii ya mkunde pori inafanya kazi ni kwenda haja ndogo mara nyingi kuliko kawaida. • Dalili nyingine ni tumbo kuvuta sana chini ya kitovu. Usipoona dalili hizi usiogope maana ukubwa wa tatizo unatofautiana. ANGALIZO KWA WANAWAKE WATAKAOTUMIA KWA AJILI YA UZAZI, Ukinywa dawa hii hakikisha siku za hatari unakutana na mwenzi wako...na baada ya hapo usitumie dawa mpaka upime mimba kwanza maana mimba nyingine dalili zake huchelewa kuonekana hivyo unaweza ukanywa tena mimba kama imeingia ikatoka. Wajawazito hawaruhusiwi kutumia. MATUMIZ CHUKUA MIZIZ

RAHA YA KUWA NA MWANAMKE MWEUSI KWENYE MAHUSIANO

Nilikuwaga sielewi kwanini hawa wanawake weusi aka blacks wanasifiwa sana?. Jaman hii type ni raha sana kudate nayo unakuwa huna stress kwanza hawana vizinga vya kizembe zembe, wanaridhika hata wakipewa kitu kidogo, yani wanajua kupenda na wengi wana true love. Sijamaliza bado, wanawake weusi wanajua nini maana ya mapenzi, wanajua kukaa na mwanaume halafu pia wanajituma sana akija ghetto anafanya kila kitu hadi kubrash viatu.  Ukija kwenye kule kwa 6x6 sio wachoyo kukupa na wanajua balaa ni mafundi na hawana maringo kabisa.  Shida ya hizi rangi nyeupe ni kwamba zina maringo sana na wanavizinga sana unakuta dada kaupele kadogo kameota anataka dawa halafu utasikia 50k dawa ya uson wtf?? Hawa mademu weupe wana vizinga sana halafu wengi ni malaya sana. Nasema haya coz me nilikuwa mhanga sana wa hizi type nyeupe ila toka nianze kula hizi nyeusi mmeona utofauti mkubwa sana mpaka nimeanza kuwaelewa mablacks yani hawana complications. Popote mlipo nyie wanawake weusi agizeni mirinda