Skip to main content

SIMULIZI; MAMA USILIE KWANI UKIAMKA ASUBUHI SISI TUTAKUA TUMELALA!

Wote tulikua tunaona mambo aliyokua anafanya Kaka yetu, si kwamba hatukua tunaweza kumuambia hapana, ni kama kila mtu alikua akimchukia mke wake ingawa hatukuwa na sababu yoyote. Mara kadhaa Mama alienda na kumtukana lakini wifi alivumilia na hakusema chochote. Kaka yangu alikua akimpelekea wanawake mpaka ndani lakini wifi alivumilia, mimi nilikua naishi kwa Kaka na niliona na kuumia.

Mara kadhaa alipochoka na kutaka kuondoka Kaka alimuambia aondoke lakini amuachie wanae. Mungu aliwabariki watoto watatu, wakike wawili na wakiume mmoja, wifi alivumilia na kukubali kuteseka kwaajili ya wanae. Kipindi hicho mimi nilikua darasa la saba hivyo kidogo nilikua napatana na wifi kwani kweli sikuwahi kumuona na kosa lolote na nilishangaa ni kwa namna gani ndugu zangu wengine walikua wanamchukia.

Siku moja nilikua nimatoka shule nakumbuka ndiyo nilitoka kufanya mtihani wa taifa kumaliza darasa la saba. Nilipofika nyumbani kwa Kaka ambapo mimi nilikua nikiishi nilikuta kuna watu wengi wamejaa. Kwa kuangalia tu nilistua kwani ilionekana kama msiba, nilitembea kwa harakaharaka na kufika pale. Nilimuona Mama amezimia na Kaka anapepewa analia kama mtoto mdogo, nilianza kuwaza ni nani kafariki wanalia hivyo.

Hakuna mtu aliyeniambia chochote, nilianza kuuliza na kuuliza ndipo nilipopatiwa habari. Watoto wote wa Kaka yangu walikua wamefariki, nilishindwa kuelewa sikutaka kuamini, niliendelea kuuliza nini kilikua kimetokea ndipo Dada yangu ninayemfuatia alinionyesha Barua. Kuona tu nilijua muandiko, ulikua ni wa mtoto wa kwanza wa Kaka yangu ambaye alikua ni kama mdogo wangu. Alikua na miaka 12, siku hiyo haikua siku ya shule kwao kwani sisi tulikua tunafanya mtihani wa Taifa, iliandikwa.

“Kwako Mama, Sikamoo. Tunakuandikia hii barua kwakua tunakupenda sana, mimi na wadogo zangu tumeona namna unvayoteseka kwaajili yetu. Baba anakupiga na kukunyanyasa kila siku, tunajua umechoka na unataka kuondoka lakini kwakua unaogopa Baba atatutesa basi umeamua kubaki. Sisi tumeamua kuondoka ili wewe uishi vizuri, sisi tunaenda sehemu nzuri kukusubiri.

Mama tunashukuru kwa kutulinda miaka yote hiyo lakini kama tukikuacha na Baba basi atakuua na sisi hatutapata tena Mama kama wewe. Hatutaki kulelewa na Mama wa Kambo. Mama usilie kwani ukiamka asubuhi sisi tutakua tumelala, usijali Mama huko kwa Mungu tutakua salama, mimi nitawalinda wadogo zangu, usiogope tena unaweza kuondoka sasa kwani Baba hatakutishia tena, sisi hawezi kutudhuru. Kwa heri Mama tunaomba umuache Baba.”

Barua ile ilishia hapo, watoto wa Kaka walikaa na kuona kuwa njia pekee ya kumuokoa Mama yao na mateso ya Kaka ni kwa wao kunywa sumu. Walinunua sumu ya Panya mjini na kuweka kwenyeJuice wote wakanywa usiku na asubuhi walikua wamekwisha fariki, mmoja alikua na miaka 13, 9 na wa mwisho miaka 6. Hakuna liyetaka kuamini lakini ilikua ni kweli, Kaka alipoteza watoto wake wote kwaajili ya kumnyanyasa mke wake.

Siku ile kila mtu alimuangalia Kaka kama shetani, wifi alilia na kulia na kila wakati alijilaumu ni kwanini hakuchukua hatua. Ni kwanini hakutoroka na watoto wake au hata hakwenda Polisi. Baada ya mazishi aliondoka na kurudi kwao, Kaka alibaki mpweke na wiki mbili tu baada ya mazishi ya wanae kutokana na msongo wa mawazo Kaka alijipiga risasi na kufa.

Ni miaka ziadi ya kumi imepita lakini mpaka leo familia yetu haiko sawa, Mama yangu amekua kama chizi, ndugu zangu wengine nao hakuna mwenye ndoa ya maana, mimi ndiyo nimaliza chuo, lakini sina hata mpenzi. Kila siku nimekua nikijilaumu kutokana na hili tukio nikiamini labda ningefanya kitu mambo yangekua tofauti. Nimeamua kukiandika labda na mimi nitapata nafuu ya maisha kwani sina furaha sina amani katika moyo wangu.

****MWISHO

Comments

Popular posts from this blog

MKUNDE PORI KIBOKO YA UZAZI | TASA

MIZIZI YA MKUNDE PORI NA FAIDA ZAKE ■ Inasafisha kizazi ■ Inazibua mirija iliyoziba ■ Inaondoa sumu kwa wale waliotumia sindano za uzazi/vidonge vya uzazi. ■ Inakomaza mayai kwa wale wenye tatizo la mayai kutokukomaa na kusababisha mayai kutokupevuka ■ Inasogeza kizazi karibu kwa wale ambao vizazi vyao vipo mbali ■ Majani ya mkunde pori pia ni dawa ya kuongeza nguvu za kiume • Dalili mojawapo itakayokufanya ujue dawa hii ya mkunde pori inafanya kazi ni kwenda haja ndogo mara nyingi kuliko kawaida. • Dalili nyingine ni tumbo kuvuta sana chini ya kitovu. Usipoona dalili hizi usiogope maana ukubwa wa tatizo unatofautiana. ANGALIZO KWA WANAWAKE WATAKAOTUMIA KWA AJILI YA UZAZI, Ukinywa dawa hii hakikisha siku za hatari unakutana na mwenzi wako...na baada ya hapo usitumie dawa mpaka upime mimba kwanza maana mimba nyingine dalili zake huchelewa kuonekana hivyo unaweza ukanywa tena mimba kama imeingia ikatoka. Wajawazito hawaruhusiwi kutumia. MATUMIZ CHUKUA MIZIZ...

RAHA YA KUWA NA MWANAMKE MWEUSI KWENYE MAHUSIANO

Nilikuwaga sielewi kwanini hawa wanawake weusi aka blacks wanasifiwa sana?. Jaman hii type ni raha sana kudate nayo unakuwa huna stress kwanza hawana vizinga vya kizembe zembe, wanaridhika hata wakipewa kitu kidogo, yani wanajua kupenda na wengi wana true love. Sijamaliza bado, wanawake weusi wanajua nini maana ya mapenzi, wanajua kukaa na mwanaume halafu pia wanajituma sana akija ghetto anafanya kila kitu hadi kubrash viatu.  Ukija kwenye kule kwa 6x6 sio wachoyo kukupa na wanajua balaa ni mafundi na hawana maringo kabisa.  Shida ya hizi rangi nyeupe ni kwamba zina maringo sana na wanavizinga sana unakuta dada kaupele kadogo kameota anataka dawa halafu utasikia 50k dawa ya uson wtf?? Hawa mademu weupe wana vizinga sana halafu wengi ni malaya sana. Nasema haya coz me nilikuwa mhanga sana wa hizi type nyeupe ila toka nianze kula hizi nyeusi mmeona utofauti mkubwa sana mpaka nimeanza kuwaelewa mablacks yani hawana complications. Popote mlipo nyie wanawake weusi agizen...

USIMUAMINI KAMWE....!!

Dada zangu naomba niandike kwa sauti kubwa kabisa mnielewe maana aisee mnadanganyika na uongo mwingine mpaka mnanpia hasira ipo siku nitavunja simu yangu hapa na hali ilivyo ngumu! Iko hivi, kama una mpenzi wako, mpo kwenye mahusiano kwa zaidi ya miezi mitatu, narudia zaidi ya miezi mitatu, hajawahi kukupeleka kwake, mechi anataka mkapigie gest au nyumbani kwako. Ukitaka kwenda kwake anaanza sijui pale wambea wengi, mara bado naishi kwetu, mara naishi na wadogo zangu, mara kuna wageni wengi sijui nini? Kuna mwingine kaambiwa eti nyumba ina choo cha nnje utasumbuka na yeye akaamini. Unakuta mwanaume anakupa visababau sababu vya kijinga jinga ambavyo havieleweki, mwanaume anafanya kazi lakini hataki kabisa ujue kwao. Hata ukimuambia kuwa nionyeshe basi nyumba ilipo hata kama sitafika niingie hataki. Lakini sasa na hapa ndiyo mnadanganywa mwanaume huyu huyu unaweza kumpigia simu hata saa nane usiku tena wakati mwingine Video call basi huyu ana mke kabisa au mwanamke anaishi naye. Wan...